Tanzania hii leo inaadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa huko jijini Dodoma, ambapo mbali na viongozi wengine watakaohudhuria kilele cha sherehe hizo, mgeni rasmi atakuwa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Wakati maadhimisho haya yakifanyika, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema, katika kipindi cha mwaka mmoja, changamoto zaidi ya kumi za muunganamo zimepatiwa ufumbuzi.