Search

Search books by typing book title or Authour

NEWS&EVENTS
SUGGESTION BOX
JOB OPORTUNITY

Download Documents

Jarida la maktaba
ZLS Policy
ZLS Brochure
ZLS ORG Structure
ZLS law
Customer Care Contract

Library workshop

Staff Training
User Training
Teacher library Training
Children programe
Inservice Training

Quick Links

Our Donors
Open Access
Wema
Staff mail
E-learning
Free books
E-library
Online Catalogue

Library links

Central Library IIT Kharagpur
Tanzania library board
Library of Congress

Library working Days

From Monday To satarday
Sunday ........... Closed
Library working hour
From 8:30 a.m to 18:00 p.m

Online user's counter

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

2018-06-26 06:31:26


Maelezo ya nafasi za kazi zilizotolewa na tume ya utumishi Serikalini Zanzibar

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. WALIMU WA SHAHADA YA KWANZA SANAA - Nafasi tatu (3) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu ya Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. WALIMU WA STASHAHADA SANAA - Nafasi nane (8) Unguja na Nafasi mbili (2) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ualimu ya Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. WALIMU WA CHETI SANAA – Nafasi hamsini (50) Unguja na Nafasi kumi na tatu (13) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. WALIMU WA SHAHADA YA KWANZA SAYANSI
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu ya Sayansi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. WALIMU WA STASHAHADA SAYANSI
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ualimu ya Sayansi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. MUHUDUMU DARAJA LA III – Nafasi moja (1) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya sekondari.
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaweza kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini wakati wa saa za kazi.
• Kwa Waombaji walioko Pemba wanaweza kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma iliopo Chake Chake – Pemba.
• Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 03 Julai, 2018 wakati wa saa za kazi.
• Tangazo hili pia linapatikana katika Tovuti WWW.LPS.GO.TZ

Copied from www.lps.go.tz